Job 3:16-21


16 aAu kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu,
kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?

17 bHuko waovu huacha kusumbua
na huko waliochoka hupumzika.

18 cWafungwa nao hufurahia utulivu wao,
hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa.

19 dWadogo na wakubwa wamo humo,
na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake.


20 e“Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni,
na hao wenye uchungu kupewa uhai,

21 fwale wanaotamani kifo ambacho hakiji,
wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa,
Copyright information for SwhKC